KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema chama chake hakina muda wa kulumbana na vyama vya upinzani, kwani wajibu wake ni kuchapa kazi. Kinana aliyasema hayo jusi, wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kahama mjini, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Kanda ya Ziwa.
“Acheni wao wapige kelele, lakini CCM inatekeleza ilani yake kikamilifu kwa kufungua fursa za kiuchumi na hata kuwapatia ajira vijana wetu,” alisema.
Kiongozi huyo wa chama aliisifu China kutokana na mchango wake katika kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kwamba kwa muda mrefu nchi hiyo imekuwa ikijenga miradi mbalimbali nchini.
“Hii ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao utafanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China,” alisema.
Miradi mingine iliyojengwa na China ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Kiwanda cha Nguo Urafiki, Uwanja wa Taifa wa kisasa wa mpira pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Ally Rufunga, alisema kuwa mkoa wake wamejipanga kutangaza fursa za uwekezaji ambapo zaidi ya vijana 1,000 watanufaika.
Akizungumza katika mikutano hiyo, Dk. Rufunga alisema mkoa wake uliunda kamati ya uwekezaji ya mkoa na kufanya mawasiliano na ubalozi wa China, ambapo ulionyesha nia ya kuwekeza mapema mwaka huu.
“Nilifanya mawasiliano na Balozi wa China, Dk. Lu, ambapo aliweza kuyakaribisha makampuni makubwa matatu kutoka China na sasa ujenzi unaendelea Shinyanga,” alisema.
Alisema hiyo ni pamoja na Kampuni ya Xing Hua Investment Ltd, ambayo inajenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama.
“Pia kinajengwa kiwanda cha nyuzi, mafuta ya pamba na nguo pamoja na chuo cha kilimo ambavyo hadi kufika Desemba mwaka huu, vitakuwa vimekamilika,” alisema Dk. Rufunga.
Alisema kutokana na mipango, hasa katika usimamizi na utekelezaji wa ilani ya CCM hadi kufikia mwaka 2015, Mkoa wa Shinyanga utakuwa na viwanda 25.
-Mtanzania