Like Us On Facebook

JAMBAZI SUGU LAPIGWA RISASI NA POLISI NA KUUWAWA JIJINI DAR.

              Jeshi la polisi kikosi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumuua mmoja kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mara baada ya kurushiana risasi na polisi eneo la SUKITA jijini Dar es Salaam. 

Tukio hilo limetoke maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam. 

 
MTU ANAEDHANIWA NI JAMBAZI BAADA YA KUUAWA NA POLISI LEO ENEO LA SUKITA JIJINI DAR 

 
HAPA NI BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA 
 
MOJA KATI YA WATU WANAODAIWA KUPORA FEDHA VINGUNGUTI BAADA YA KUUAWA NA POLISI 
Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la tukio. 

Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao, alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea kusikojulikana

 
KIKOSI CHA DEFENDER CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKOSI CHA POLISI MAGOMENI
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari