Like Us On Facebook

JACK DUSTAN MCHARUKO UGHAIBUNI

                                                               Jacqueline Dustan.
STAA wa Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan ameonyesha tabia za mcharuko akiwa pande za Dubai  kwa kupiga picha katika mikao tata na mrembo mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwajabu Juma.
Jacqueline ambaye ametimkia nchini humo hivi karibuni, amezua zogo mtandaoni baada ya wadau mbalimbali kumponda kwa kuonesha tabia chafu katika nchi za watu. Alipouulizwa kuhusu picha hiyo kuzagaa mtandaoni, hakujali:
“Jamani Wabongo msione jambo, sasa hii picha hapa ina ubaya gani? Mbona ni pozi tu la kawaida tu wala sioni kitu chochote ambacho kinaweza kuwashangaza,” aliandika Jacqueline. 

-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari