Msanii wa sinema za Kibongo, Irene Paul amesema ameridhishwa na uwezo wa mkali wa sinema za Kinigeria, Joseph Van Vicker akidai ni jasiri na mjuzi sana katika scene za mapenzi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Irene alisema kuwa pamoja na kuigiza naye kwa mara ya kwanza ‘scene ya on bed’ lakini Vicker alionesha uzoefu wa hali ya juu utadhani wanafahamiana kitambo, jambo lililomshangaza na kujikuta akiingiwa na woga.
“Jamaa utadhani tunafahamiana, alinikabili kitandani kwa kiwango kikubwa sana, nilipata hofu kubwa mno. Van anajua kuigiza jamani, kwangu hii ni bahati ambayo namshukuru Mungu kuipata, wengi waliililia,” alisema Paul.
Van aliibuka Bongo na kuondoka wiki iliyopita kwa ajili ya kushuti sinema moja na wasanii wa nyumbani ambayo bado haijapatiwa jina.