MSANII wa filamu nchini na muziki wa Injili, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, amesema kwamba kukata kwake viuno jukwaani akiimba ni imani yake na jamii iache kumsimanga kwa maneno. Dokii aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha runinga cha TBC katika Funguka, kuhusu kukata kwake viono katika nyimbo za dini.“Hakuna anayeweza kumhukumu mtu, ila ni Mungu pekee na suala la kupendezwa au kutopendezwa na kitendo changu pindi niwapo jukwaani ni imani yangu inaniruhusu kufanya hivyo.
“Mimi ni Mlokole na nampenda Mungu kuliko watu wanavyofikiria, nimeshasikia maneno yakidai nimeachana na wokovu, lakini hawajui suala la wokovu ni la mtu binafsi na Mungu wake,” alisema Dokii.
Alisema jamii isipende kuingiza tamaduni za nchi na dini, kwani katika nchi dini zilikoanzia hayo ni mambo ya kawaida na ndiyo imani yao inavyowaambia.