Like Us On Facebook

DIWANI WA CHADEMA AMTOROSHA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA KUMGEUZA MKE HUKO MBEYA...!

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya
 DIWANI wa kata ya Kiwira mkoani Mbeya, Laurent Mwakalibule (Chadema) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya sekondari ya Kiwira na kufanya naye mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) mwenye miaka 18 alitoroshwa na diwani huyo Septemba 12 mwaka huu.
“Majira ya saa 1:30 usiku katika kitongoji cha Kibumbe kata ya Kiwira Kati, Mkulima Raphael Frank(42) na mkewe Susan (38) wakiwa nyumbani kwao waligundua mtoto wao huyo hayupo ndipo jitihada za kumtafuta zilianza bila mafanikio,” alisema Kamanda huyo.
Alisema siku iliyofuata saa 12 jioni wazazi hao walitoa taarifa polisi baada ya kuona mtoto wao hakulala nyumbani hali ambayo si kawaida.
Hata hivyo saa 3:00 usiku wa Ijumaa, mtoto huyo alirejea nyumbani na baada ya kuhojiwa na wazazi wake alijibu alikuwa kwa diwani huyo mwenye miaka 28.
“Aliwaeleza wazazi wake kuwa alilala na diwani huyo katika nyumba ya mdogo wake ambaye jina lake halijajulikana na kabla ya kukutana waliwasiliana kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Athuman.
Kamanda huyo alisema diwani huyo amekamatwa na upelelezi unaendelea. Kutokana na tukio hilo, Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kujiepusha na madhara ya kufanya mapenzi kwani ni hatari kwa afya zao na maisha yao ya baadaye.

SOURCE: HABARI LEO
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari