Hit maker wa Sio Mimi aka Pombe yangu,  Madee amesema hadi sasa ameshaingiza zaidi ya shilingi milioni 130  kutokana na show mbalimbali alizopata hivi karibuni tangu aachie wimbo  wake  huo.
Madee amesema pamoja na show za kawaida,  makampuni ya simu yameshamsainisha show zaidi ya 12 ambazo zimekuwa  zikimpa mkwanja wa nguvu.
Akiongea na mwandishi wetu, Madee  amesema pia muziki wake umetoa fursa kwa vijana wa Tip Top Connection  ambao amekuwa akifanya nao kazi katika show mbalimbali.
“Nimekua nikiingiza Milioni 2 hadi 3 kwa  wiki kutokana na Pombe Yangu. Ni tofauti na awali wakati tunaanza  muziki kwa sasa ukifanya wimbo ukawa mkali basi ujue pesa zipo  zinakusubiri. Pamoja na hayo wimbo ya Pombe Yangu umetoa fursa kwa  vijana ambao nakuwanao kwenye show zang. Filamu ya “Pombe Yangu” pia  imeajiri vijana,watu wametengeneza T-Shirt ‘Nani kamwaga Pombe Yangu’.  Hiyo ni fursa wameitumia kupitia Pombe Yangu, alisema Madee.



 
 
 
 
 
 
