"Unajua Shija domo lake lilikuwa zege kumbe alikuwa ananitaka lakini akashindwa kuongea hadi mwenzake Sajuki (marehemu mumewe) alipotuma maombi na kusikilizwa, Baada ya Sajuki kukamilisha kila kitu na kuwa mke na mume ndiyo aliponitonya kuhusu habari ya Shija kuwa wakati wananifuata kumbe alikuwa ananitaka ila marehemu Sajuki akawa mjanja." alisema Wastara
Shija mwenyewe anasema kuwa wakati huo alipokuwa anamtaka Wastara yeye alikuwa makini na kazi hasa utayarishaji wa filamu na suala la mapenzi lilikuwa la ziada.