Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao ni wa vijiji vya Singa, Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.
Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita