Akizungumza na gazeti la HabariLeo juzi katika Viwanja vya Maonesho vya Nane-Nane, Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Radhia Rajab alisema kozi hizo mpya zinatarajiwa kuanza muhula wa masomo wa mwaka 2013/2014 unaotarajia kuanza Oktoba mwaka huu.
Alisema baadhi ya kozi za:Cheti zitakazotolewa ni pamoja nai: Uandishi wa Habari, Uhasibu, Masoko, Utalii, Ufugaji Nyuki, Utengenezaji wa Matangazo, Uongozi na Ustawi wa Jamii.
Diploma ni pamoja na: Uuguzi, Ufamasia, Mawasiliano kwa Umma, Utengenezaji wa filamu, Utaalamu wa Maabara, Kiswahili, Uhasibu na nyinginezo.
Alisema lengo la kozi hizo ni kuona wanafunzi wengi walio mitaani wanajiunga na chuo hicho ambapo sifa kubwa ni kuwa na kiwango cha ufaulu wa alama D katika masomo manne.