Mama na mwanae wameuawa kikatili baada ya kukatwa mapanga na baadhi ya viungo vyao kuchomwa moto katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina lililotokea mkoani Shinyanga.
Wanawake hao vikongwe mtu na mtoto wake ni Jadi Temi (90) na mwanae Samara Mathias (70) wakazi wa kijiji cha Ikonda wilayani Shinyanga.
Wawili hao walishambuliwa na kuuawa juzi na watu wasiojulikana wakiwa wamekaa nje ya nyumba yao wakiota moto na kufurahi chakula cha usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinha Kihenya Kihenya, alisema vikongwe walishambuliwa na mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na kufa papo hapo huku baadhi ya viungo vya Samara vikitupwa kwenye moto uliokuwa jirani.
Kihenya alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa saa 2:00 usiku katika kijiji cha Ikonda wilayani Shinyanga, wakati wawili hao wanaoishi peke yao wakila chakula na kuota moto.
Kihenya alifafanua kuwa mara baada ya kushambulia na kuua wauaji hao wakikata kichwa cha Samara, kiganja cha mkono wa kushoto na mguu wa kulia na kuvitupa kwenye moto uliokuwa jirani .
Alisema wauaji hawakuiba chochote na kuna wasiwasi kuwa mauaji hayo yamefanywa kutokana na ushirikina .