Like Us On Facebook

LICHA YA IDADI YA WATU KUFA IKIZIDI KUONGEZEKA MISRI..!!! WAFUASI WA MORSI WAPANGA KUANDAMANA TENA LEO


Maandamano zaidi yamepangwa kuendelea mjini Cairo Misri, ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wananuia kuandamana baada ya sala ya Ijumaa.

Haya yanajiri siku mbili baada ya maafisa wa usalama Misri kuvunja kambi walimokua wafuasi wa Vuguvugu la Muslim Brotherhood ambapo katika makabiliano hayo zaidi ya watu 500 waliuawa na maelfu kujeruhiwa.



Wakati huo huo serikali ya mpito ya Misri imemlalamikia Rais wa Marekani Barack Obama kwa kulaani mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana na amesitisha mazoezi ya pamoja na jeshi la Misri ingawa hakutangaza ikiwa Marekani itasimamisha msaada wa dola bilioni 1.3 kwa jeshi la Misri.

Kiongozi wa Mpito wa Misri amesema matamshi ya Obama yanawapa nguvu makundi ya wanamgambo kuendelea kutekeleza vitendo vya kigaidi.Usalama umeendelea kuimarishwa mjini Cairo, huku magari ya kivita yakionekana kushika doria.

Muslim Brotherhood imewaomba wafuasi wake kujitokeza kwa maandamano baada ya sala ya Ijumaa wakiitaja kama siku ya hasira. Upande unaompinga Bw. Morsi umeomba maandamano kupinga vuguvugu la Mosri. Kuna wito watu kulinda makanisa na makaazi nchini Misri. Wakristo wa madhehebu ya Copt wamelengwa katika siku za karibuni.

Makanisa 25, makaazi na biashara za Wakristo zililengwa na wafuasi wa makundi ya kiisilamu hapo Jumatano na Alhamisi. Kuna hofu ya umwagikaji zaidi wa damu baada ya serikali kuonya kuwa polisi watatumia risasi kujilinda na kulinda taasisi za serikali.

-bbc swahili
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari