Like Us On Facebook

HUYU NDIYE KIJANA MPIGANIA HAKI ZA MASHOGA ALIYE UAWA KIKATILI,CAMEROON.

Mpigania haki za mashoga nchini Cameroon amekutwa amekufa nyumbani kwake Yaounde baada ya kuteswa, Wapigania Haki za Binadamu wamesema.

Mwili wa Eric Lembembe ulikutwa kwenye jiji hilo mnamo siku ya Jumatatu huku ukionekana alikuwa ameteswa vibaya sana, kundi hilo lilisema kwenye maelezo yao siku ya Jumanne.

“Maraiki wa Lembembe waliukuta mwili wake mnamo siku ya Jumatatu jioni. Kwa mujibu wa rafiki zake shingo yake ilivunjwa na uso wake, mikono na miguu viliunguzwa moto kwa kutumia pasi,” taarifa ilisema.

Shirika hilo limeelezea kitendo hicho kama ni cha “mauwaji”na kuzitaka mamlaka husika kuendelea kufanya uchunguzi wa kina

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari