Like Us On Facebook

FAIDA KUMI ZA KIAFYA ZA KUFANYA MAPENZI

Hii ni kwa wakubwa tu!!!....inawezekana wengi wetu tunafanya mapenzi kwa malengo tafauti na faida hizi zilizotajwa hapa chini. Ila achilia mbali sababu zako zakufanya ngono hizi nifaida za kiafya ambazo unaweza zipata.. Kumbuka ukimwi upo na unaua.
   1. HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA MSONGO WA MAWAZO NA SHINIKIZO LA DAMU
 

Kwa kufanya ngono kunaweza kukupunguzia msongo wa mawazo na shinikizo la damu. Tafiti hii ilifanywa na huko Scotland, ambapo watafiti waliwatafiti wanawake 24 na wanaume 22, ambao walikua wakihifadhi kumbukumbu za mara ambazo wamefanya ngono.
Watafiti waliwaweka kundi hilo la utafiti katika hali yakuwatia msongo wa mawazo kama kuongea kwenye umati, kufanya hesabu kwa sauti na kufuatilia shinikizo lao la damu (mapigo ya moyo)  Matokeo yalionyesha watu walio walifanya mapenzi kabla walimudu kutawala msongo wa mawazo kuliko wale ambao hawakufanya.

2   2.HUONGEZA KINGA YA MWILI

Kufanya ngono mara moja au mbili kwa wiki kunahusishwa na kuongezeka kwa kinga ya mwili iitwayo kwa kitaalamu Immunoglobulin A (IgA) ambayo inauwezo wa kukulinda na homa na maambukizi mengine.
Utafiti wa chuo cha Wilkes uliohusisha wanafunzi 112 walio rekodi mara ambazo wamefanya ngono, ulionyesha kua wale waliofanya ngono mara moja au mara mbili kwa wiki walikua na kiwango kikubwa cha IgA kuliko wanafunzi wengine.


3. NGONO HUCHOMA KAROLI

Kufanya ngono kwa dakika 30 kutakuwezesha kuchoma karoli 85, kiwango hiki kinaweza kuonekana kua ni kidogo ila iwapo utarudia zaidi ya mara moja basi utakua umepunguza karoli za kutosha na hata kupunguza uzito.
Mtaalamu wa mambo ya ngono Patti Britton anasema ngono ni aina nzuri ya mazoezi kwasababu huhusisha matumizi ya nguvu na saikolojia.


4. HUBORESHA AFYA YA MOYO

Utafiti uliofanyika kwa miaka 20 huko uingereza unaonyesha kua wanaume wanao fanya ngono mara mbili au zaidi kwa wiki wanafaida zaidi ya nusu ya kutopata mshtuko wa moyo zaidi ya wale waliofanya ngono chini ya mara moja kwa mwezi.
Pamoja na mashaka waliyo nayo watu wenye umri mkubwa ya kwamba ngono yaweza kuwasababisha kupata sroke hakuna tafiti iliyoweza kuthibitisha hilo.


5. HUONGEZA KUJIAMINI

Watafiti wa chuo kikuu cha texas wamegundua kua katika sababu 237 za wanaume kufanya ngono, ‘kuongeza kiwango cha kujiamini’ nimoja ya sababu hizo.
Mtaalamu mshauri wa mambo ya ngono,ndoa na familia anakubaliana na tafiti hizo, anasema moja ya sababu ya watu kufanya ngono ni kutaka kujisikia vizuri kuhusu wao, pia anachagiza kua ngono bora huanza kwa kujiamini.
Ila pia anashauri kujiamini kunaanza na wewe mwenyewe, na huna haja ya kufanya ngono mara nyingi ili ujisikie vizuri na kujiamini, ila kama tayari unajiamini ngono inaweza kukusaidia kujiamini zaidi.

6. HUONGEZA UPENDO

Tafiti zinzonyesha kua kufanya ngono kunaongeza homini za oxytocin, zijulikanazo kama homoni za upendo zinazosaidia watu kupendana zaidi na kuaminiana.
Utafitiuliofanyika kwa wanawake 59, ambapo mtafiti alipima kiwango cha oxytocin kabla na baada ya wanawake hao kuwakumbatia wapenzi wao, ulionyesha wanawake walikua na kiwango kikubwa cha oxytocin baada ya kugusana na wapenzi wao.

7. HUWEZA PUNGUZA  MAUMIVU

Pia kwa kiwango kikubwa homoni ya Oxytocin inaongeza vimauliza maumivu mwilini viitwavyo endorphins.
 Katika utafiti watu 48 walinusishwa mvuke wa oxytocin na wakachomwa vidole na walionyesha uvumilivu mkubwa wa maumivu.

 

8. HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KANSA YA MAKENDE

Utafiti unaonyesha kua kufika mshindo (kupiz) mara kwa mara kwa wanaume kunapunguza uwezekano wakupata kansa ya makende maishani mwao, hususani katika umri wa miaka 20 na kitu.

Utafiti uliochapishwa katika kitabu cha Journal of the American Medical Association uligundua kua wanume waliofika mshindo(kupiz) mara 21 na zaidi kwa mwezi wanauwezekano mdogo wakupata saratani ya makende zaidi yaw a wale wlio pata mshindo mara nne au saba kwa mwezi. Utafiti huu haukuprove kama mshindo au kupiz ndo sababu pekee ilitayo kansa ya makende.

9. HUIMARISHA MISULI YA UKE

Kufanya ngono mara kwa mara kwa wanawake huimarisha misuli ya uke itwaayo Pelivic nakuwafanya kufurahia mapenzi zaidi.

Soma zaidi kuhusu misuli ya Pelvic

10. HUSAIDIA KUPATAUSINGIZI MNONO

Homoni za oxytocin zinazo zalishwa mwilini wakati wakufika kileleni (mshindo) zinasaidia kukupa usingizi mwanana. Hi indo sababu ya baadhi ya wanaume hulala baada tu ya kufika kileleni.


Pamoja na Haya yote kumbukeni Ukimwi unaua.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari