Like Us On Facebook

VIDEO:MSICHANA ACHAPWA VIBOKO AKIDAIWA KUVAA NGUO FUPI HUKO MKOANI ARUSHA

Msichana aliyekuwa amevaa nguo fupi amejikukuta akizomewa na kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la NMC jijini Arusha.
Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamariawema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.
 Mwandishi wetu Halfani Lihundi  kutoka arusha alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema,  watu walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo.
Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
VIDEO HII HAPA CHINI
 
SOURCE:ITV


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari